Karibu Karibu kwenye Tovuti rasmi ya Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu. Ofisi hii inatambua umuhimu wa taarifa kwa wananchi katika kuibua mawazo mapya yanayoweza kuchangia maen

Tovuti Rasmi Ya Ikulu

Karibu

Karibu kwenye Tovuti rasmi ya Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa , Ikulu. Ofisi hii inatambua umuhimu wa taarifa kwa wananchi katika kuibua mawazo mapya yanayoweza kuchangia maendeleo ya nchi. Tovuti hii imetayarishwa ili  kukurahisishia kupata  taarifa bure kuhusu shughuli za kila siku za Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa zinazoboreshwa mara kwa mara.

Kwa kuzingatia dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutaka taarifa sahihi ziwafikie wananchi, Asasi mbalimbali zisizo za Serikali, Kitaifa na Kimataifa na watoa maamuzi ya kisera  kwa wakati na kwa urahisi  wakati huo huo kuwahakikishia wananchi usalama na faragha.

Kazi

Mwaka 1976 alijiunga na Chuo Kikuu cha Maofisa wa Jeshi Monduli na kutunukiwa Cheo cha Luteni Kanali na baadaye kuwa Mkufunzi Mkuu na Kamisaa wa Siasa katika chuo hicho. Mheshimiwa Kikwete amefanya kazi katika Chama cha Mapinduzi kwa nyadhifa mbalimbali kwenye mikoa ya Singida na Tabora na  wilaya za Nachingwea na Masasi.

Mwaka 1988 aliteuliwa kuwa Mbunge na Naibu Waziri wa Nishati na Madini. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa  Jimbo la Bagamoyo na akateuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini. Nyadhifa nyingine alizoshika ni Waziri wa Fedha mwaka 1994 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.

Alishika rasmi wadhifa wa urais mwaka  2005 na kuchaguliwa tena 2010 kwa muhula mwingine wa  miaka mitano.

Elimu

Alipata elimu ya msingi na ya kati katika shule za Msoga na St. John Bosco Lugoba kati ya mwaka 1958 na 1965. Aidha, alipata elimu ya sekondari katika shule za sekondari za Kibaha (1966 – 1969) na Tanga (1970 – 1971).Alihitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1975 na kupata Shahada ya Uchumi,

Nyadhifa nyengine

Mwanyekiti wa Viongozi wa Afrika Kupambana na Malaria (ALMA) 2010-2011
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Januari 2010
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) Mwaka 2008

Anuani ya Ikulu

Ofisi ya Rais Ikulu,

1Barabara ya Barack Obama,

11400 Dar es salaam

Simu : 0222116898

Simu : 0222116900/6

Nukushi: 0222113425/

2116910/2117272

Barua pepe : [email protected]
Mwenyekiti Mwenza wa Mchakato wa Helsinki kwenye Utandawazi na Demokrasia Mwaka 2004
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mwaka 2004
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika (OAU) Mwaka 1997
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mwaka 1997
Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) Mwaka 1995

Listing Details


Category ,
Keywords  

Contact Author Complete the fields below to contact this listing author.